Habari yako ndugu msomaji wangu.
Leo napenda tushirikishane mambo kadhaa kuhusu jamii yetu.mara nyingi usiku wa manane watu huwa wamelala na hata ambao hawakulala huwa wanaogopa kuzulura . Ni ajabu kidogo na nishawai kujiuliza kwanini usiku wa manane huogopwa.
Majambazi ni mara chache kufanya uharifu mchana kweupe, uovu mwingi hufanyika gizani.ijapokuwa kwa jamii ya sasa na kizazi hiki mambo yamebadilika uovu uliokuwa ukifanywa zamani nyakati za usiku ,hufanywa mchana kweupe bila hata aibu.
Ilikuwa ni nadra sana kutokea mwanamke asiyejisitiri yaani nusu utupu kuonekana mchana kweupe na hata ikitokea jamii ilimkemea .lakini kwa kizazi hiki siyo ajabu kabisa naweza kusema imebaki kidogo tu tujionee wadada wakipita vifua wazi,visiketi vya aibu.kinachonishtua zaidi jamii iko kimya hakuna anaekemea siyo ajabu kumuona mdada nusu utupu na watu wanamshangilia (usiku wa manane) kiza kimetanda hakuna anaeona.
Wako wapi wazee wa hekima ,wako wapi watumishi wanaojiita wametumwa na Mungu na kujivika majina yenye tukufu nyingi unamkuta mtu anajiita mtume,nabii,mchungaji lakini katika nyumba yake anayotumia kufanyia huduma yake kuna watu wako kana kwamba ni wauzaji wa bar. Ni hao hao wanajikuta hawaoni mwisho wanakula hata kondoo wao kwa kuwa hawakukemea tabia hiyo.Nina akili timamu na nakuambia sijapitwa na wakati kama unavodai.
Unaenda na wakati upi kuanika tupu zako hadharani?,wakati upi ? ebu sema tukusikie.jisitiri nyeti zako ni mali ya mume wako.wakati upi unaoendana nao unavaa nguo zinazomtosha mdogo wako wa mwisho? Endelea kusoma na usipuuze nakwambia toa giza usoni pako ujitafakari
Zamani wadada waliokuwa wanajiuza walikuwa wanaonekana usiku wa manane na ilikuwa ngumu kuwatambua muda wa mchana.ila usiku walijitambulisha kwa mavazi yao yaliyoacha sehemu kubwa ya miili yao wazi ili kuwatega wanaume.je wewe unayevaa mavazi hayo mchana kweupe tukuulize na wewe unajiuza au ndo huko kwenda na wakati.Huo ni usiku wa manane ninaouona kwako.jitafakari tukutane tena
malilabl.blogspot.comItaendelea...
